Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tume huru ya uchunguzi Syria yapewa mwaka mmoja zaidi

Tume huru ya uchunguzi Syria yapewa mwaka mmoja zaidi

Baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa limepitisha azimio la kuongeza kwa mwaka mmoja zaidi muda wa tume huru ya kimataifa ya uchunguzi kuhusu Syria.

Azimio hilo limepitishwa kwa kura 29 huku Sita zikipinga na nchi 12 hazikuonyesha upande wowote.

Kwa mujibu wa azimio hilo, hatua hiyo inatokana na kuendelea kuzorota kwa hali ya haki za binadamu na kibinadamu nchini Syria ambako mzozo sasa umeingia mwaka wa Tano.

Pamoja na kuongeza muda, azimio linalaanza vikali vitendo vya kigaidi vinavyofanywa na kikundi cha ISIL au Da’esh, halikadhalika matumizi ya silaha za kemikali nchini Syria.

Baraza pia limelaani kitendo cha wapiganaji mamluki kuhusika kwenye mzozo wa Syria na kuelezea wasiwasi wake mkubwa juu ya kitendo hicho kuzorotesha zaidi hali ya Syria.