Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mauaji ya Albino Malawi yachukua hatua, Tanzania nayo iimarishe:UM

Mauaji ya Albino Malawi yachukua hatua, Tanzania nayo iimarishe:UM

Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa imekaribisha mpango wa hatua tano uliotangazwa na serikali ya Malawi katika kukabiliana na mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi, Albino.

Msemaji wa ofisi hiyo Rupert Colville akizungumza Geneva, Uswisi ametaja mpango huo kuwa ni Mosi elimu kwa umma, pili, kuimarisha ulinzi wa kijamii na kuongeza polisi kwenye wilaya zenye matukio mengi zaidi, Tatu..

“Kutafiti chanzo cha tatizo hilo na viungo vya albino hutumika kwa ajili gani nan ne kutathmini sheria zilizopo na kupitisha sheria mpya iwapo italazimika ili kuhakikisha ulinzi wa Albino.”

Kuhusu Tanzania amesema wana imani na kauli ya Rais Jakaya Kikwete ya kutokomeza matukio ya mauaji ya Albino ikiwemo ofisi ya mwanasheria mkuu kuanza kuandaa mpango wa kuelimisha umma na kuondokana na ukwepaji sheria lakini..

“Hata hivyo inaonekana idadi kubwa ya waganga wa kienyeji waliokamatwa wiki chache zilizopita wameachiliwa huru. Kwa mara nyingine tena tunaomaba serikali ichukue hatua kuhakikisha uwajibikaji kwa uhalifu unaotendwa dhidi ya Albino.”