Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Alikuwa mtoto vitani miaka 10, sasa awasaidia wahanga wengine

Alikuwa mtoto vitani miaka 10, sasa awasaidia wahanga wengine

Wakati wa mjadala maalum wa Baraza la Usalama kuhusu watoto waliotumikishwa vitani, Junior Nzita Nsuami, kijana mmoja kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, amewaelezea Wanachama wa Baraza hilo mateso aliyoyapitia akiwa miongoni mwa watoto hao.

Kijana huyo alitumikishwa vitani tangu alipokuwa na umri wa miaka 12, na akajisalimisha akiwa na umri wa miaka 22. Baada ya kupitia maisha ya jeshi, na mauaji ya vita, ameanza upya masomo yake na akaanzisha asasi isiyo ya kiserikali ili kuwasaidia watoto waliotumikishwa vitani. Tayari shirika hilo linawasaidia watoto 98, na Junior anaendelea kuhamasisha jamii ili kutokomeza utumikishwaji wa watoto vitani.

Katika mahojiano na Priscilla Lecomte wa Redio ya Umoja wa Mataifa, Junior anahadithia maisha aliyoyapitia…