Skip to main content

Sanaa ya kukumbuka utumwa yazinduliwa New York

Sanaa ya kukumbuka utumwa yazinduliwa New York

Safina ya marejeo au The Ark of Return kwa kiingereza ni sanaa iliyochongwa na msanifu wa Marekani Rodney Leon ili kukumbuka daima utumwa na biashara ya utumwa kupitia bahari ya Atlantiki.

Uzinduzi huo ulifanyika kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa wakati ambapo muongo wa watu wenye asili ya kiafrika imeanza rasmi.

Katibu Mkuu Ban Ki-moon, rais wa Baraza kuu Sam Kutesa, Waziri Mkuu wa Jamaica Bi Portia Simpson Miller na Mkurugenzi wa Shirika la Sayansi Elimu na Utamaduni Irina Bokova walikuwepo kwenye hafla hiyo iliyohudhuriwa pia na mabalozi wan chi mbalimbali ikiwemo Kenya.

Kulikoni? Ungana na Priscilla Lecomte kwenye makala hiyo.