Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kuelekea uchaguzi Nigeria, Chambas awasilisha ujumbe wa Ban

Kuelekea uchaguzi Nigeria, Chambas awasilisha ujumbe wa Ban

Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwa nchi za Afrika Magharibi, Mohammed Ibn Chambas anaendelea kufuatilia kwa karibu hali nchini Nigeria wakati huu ambapo nchi hiyo inaelekea uchaguzi mkuu keshokutwa Jumamosi.

Umoja wa Mataifa kupitia Naibu Msemaji waje Farhan Haq umetolea mfano ziara ya Alhamisi ya mwakilishi huyo huko jimbo la Gombe, kaskazini mwa Nigeria kwa lengo la kukutana na viongozi husika.

Tayari ameshakutana na viongozi kadhaa wa mji wa Port Harcout jimbo la River akiwemo gavana na kiongozi kutoka tume huru ya taifa ya uchaguzi, ikiwa ni sehemu ya ziara yake nchini Nigeria iliyoanza tarehe 15 mwezi huu.

“Bwana Chambas amewapatia aliozungumza nao ujumbe wa Katibu Mkuu kuhusu uchaguzi wa amani, huru na halali. Amesihi wadau wote kujitahidi  kufanikisha suala hilo akigusia zaidi mamlaka za usalama kuzingatia zaidi weledi wanapotekeleza wajibu wao wakati na baada ya uchaguzi.”