Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Jumuiya ya kimataifa inawajibu wa kusaidia kumaliza mgogoro wa Israel na Palestine

Jumuiya ya kimataifa inawajibu wa kusaidia kumaliza mgogoro wa Israel na Palestine

Baraza la Usalama leo limekuwa na mashauriano kuhusu hali Mashariki ya Kati ambapo Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na Mratibu wa Amani katika ukanda huo Robert Serry amelihutubia baraza hilo akisema bado mvutano kati ya Palestina na Israel unaendelea kuleta madhara makubwa kwa watu  wa Gaza na  kutaka suluhu la kisiasa hima.

Bwana Serry amesema lazima pande zote zikubaliane na kurejea katika meza ya mazungumzo lakini akatoa wito kwa kwa jumuiya ya kimataifa.

(SAUTI SERRY)

"Jumuiya ya kimataifa lazima izingatie kupendekeza mkakati wa majadiliano wenye vigezo vya kufanikisha amani. Hii yaweza kuwa njia pekee ya kuwezesha malengo ya muafaka kwa  mataifa haya mawili. Amani ni jukumu la kipaumbele kwa pande katika mzozo huu."