Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kizazi hiki lazima kipate elimu juu ya utumwa: Ban

Kizazi hiki lazima kipate elimu juu ya utumwa: Ban

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban ki- Moon amesema ni muhimu kizazi hiki kifahamu madhara ya biashara ya utumwa ili kuhakikisha vitendo hivyo havijirudii katika historia ya mwanadamu kote duniani.

Akiongea katika kumbukizi ya siku hii baada ya kuzindua katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York, kumbukizi ya kudumu ya wahanga wa utumwa na biashara ya utumwa kupitia bahari ya Atlantiki Bwana Ban amesema idatra ya mawsiliano kwa uma ya Umoja wa Mataifa pamoja na shirika la elimu, sayansi na utamduni UNESCO wako tayari kufanikishe elimu hii na kusisitiza.

(SAUTI BAN)

"Kukuza uelewa kuhusu masuala haya ni hatua ya kwanza tu. Tunazihamasisha nchi wanachama kuanzisha masomo katika mitaala ya shule kuhusu vyanzo na madhara na somo la biashara ya utumwa kupitia bahari ya Atlantiki"

Lengo la kumbukizi hiyo iitwayo Safina ya marejeo ni kusaidia kuponya makovu ya utumwa wakati wahanga wanapokumbukwa