Skip to main content

Nafasi ya mwanamke katika meza ya majadiliano ni muhimu:KEWOPA

Nafasi ya mwanamke katika meza ya majadiliano ni muhimu:KEWOPA

Ushirikishwaji wa  wanawake katika maswala mbali ya kijamii ni muhimu kwa ajili ya maendeleo kwa wote. Hatua hiyo ni muhimu kwa kuwa inahakikisha  wanawakilishwa ipasavyo katika meza ya majadiliano hususan wakati huu ambapo dunia inafikia ukomo wa malengo ya maendeleo ya milenia na kuanza malengo ya maendeleo endelevu.

Hilo limedhihirisha wakati wa mahojiano kati ya Grace Kaneiya wa  Idhaa hii na wabunge kutoka Kenya walioshiriki  vikao vya hali ya wanawake kwenye  makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York.

Mmoja wao ni Cecily Mbarire, mwenyekiti wa Muungano wa wanawake wabunge nchini Kenya, KEWOPA ambaye anaanza kwa kueleza baadhi ya sheria ambazo wameweza kushiriki katika kuzipitisha bungeni.