Skip to main content

Maendeleo endelevu na ujuimuishwaji ni ufunguo wa maendeleo: Mshiriki wa mkutano

Maendeleo endelevu na ujuimuishwaji ni ufunguo wa maendeleo: Mshiriki wa mkutano

Wakati mkutano wa kupanga na kutekeleza malengo endelevu na majadiliano ya kimataifa ukiendelea katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York, ushirikishwaji wa makundi yote katika jamii na nammna ya kuyatekeleza kwa kuzingatia mahitaji ya nchi vimemulikwa.

Mkutano huo unaoleta wawakilishi wa nchi na asasi za kiraia pamoja, umejadili nafasi na ushiriki wa makundi ya kijamii mathalani wafugaji na watu wa asili. Kutoka Tanzania mwakilishi wa makundi hayo kutoka taasisi ya wafugaji na mendeleo PIDO, Martha Ntoipo ambaye pia anawakilisha jamii asilia anaelezea nafasi ya makundi hayo katika majadala huo kama anavyohojiwa na Joseph Msami .

(SAUTI MAHOJIANO)