Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WPF yapokea magari 67 kutoka Urusi

WPF yapokea magari 67 kutoka Urusi

Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) nchini Uganda limekaribisha mchango wa magari ya mzigo 67 kutoka serikali ya Urusi ambayo yatasaidia kuimarisha uwezo wake wa kusambaza chakula katika Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati. John Kibego na maelezo kamili.

(Taarifa ya John Kibego)

Magari hayo aina ya KAMAZ ni sehemu ya mchango wa kimataifa wa magari 218 wenye thamani ya US$21 milioni kutoka serikali ya Urusi. Yanakuja sanjari na warsha za mkononi, vipuri, mafundi na US$1.6 milioni za gharama za uendeshaji. Magari mengine 61 yanatarajiwa kupokewa mwishoni mwa mwezi huu.

Akipokea magari hayo kwenye ghala la Tororo Mahsariki mwa Uganda, Mkurugenzi wa WFP humo nchini, Michael Dunford ameshukuru serikali ya Urusi kwa kuitikia dharura iliopo kusaidia watu walio mizozoni.

Kulingana na WFP, mara moja magari 53 yanatumwa Sudan Kusini ambako kuna dharura kubwa sasa. Mengine yanasalia kwenye kituo cha magari cha shirika hilo katima mji mkuu wa Uganda, Kampala.