Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkutano wa kuchangia ubinadamu Syria kufanyika mwishoni mwa mwezi huu

Mkutano wa kuchangia ubinadamu Syria kufanyika mwishoni mwa mwezi huu

Mkutano wa Tatu wa kimataifa kuhusu usaidizi wa Syria  utafanyika huko nchini Kuwait tarehe 31 mwezi huu.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ndiye atakuwa mwenyekiti wa mkutano huo utaokuwa chini ya uenyeji wa kiongozi mkuu wa Kuwait Sheikh Sabah Al-Ahmad Al-Jaber Al-Sabah.

Viongozi wengine waandamizi watakaohutubia ni kutoka ofisi ya Umoja wa Mataifa ya misaada ya kibinadamu , OCHA halikadhalika shirika linalohusika na wakimbizi, UNHCR na lile la mpango wa maendeleo la Umoja wa Mataifa, UNDP

Mkutano huo unalenga kuchangisha fedha za kukikidhi mahitaji yaliyoanishwa kwenye mpango wa hatua kwa Syria wa mwaka 2015 halikadhalika mpango wa usaidizi kwa wakimbizi wa Syria kwa mwaka 2015/2016.

Umoja wa Mataifa unasema mzozo wa Syria unapoingia mwaka wa Tano, watu zaidi ya Milioni 12 wamesalia katika mahitaji makubwa ya usaidizi.

Takribani nusu ya raia wa Syria wamelazimika kukimbia makaziyao ambapo baadhi ni wakimbizi wa ndani ilhali wengine wanaishi ugenini huko Lebanon, Jordan, Uturuki, Iraq na Misri.