Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ushairi na nafasi yake katika maridhiano nchini Somalia

Ushairi na nafasi yake katika maridhiano nchini Somalia

Somalia, nchi inayojulikana duniani kwa utamaduni wa mashairi. Hivi sasa sanaa hiyo inatumika kuimarisha amani na maridhiano kutokana na vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyoanza zaidi ya miongo miwili iliyopita.

Mabingwa wa utunzi na ughani wanachukua nafasi yao huku harakati zikiendelea ili kurithisha tasnia hiyo adhimu kwa vijana ambapo tayari jukwaa la wasani nchini humo linataka ushahiri ufundishwe hadi Chuo Kikuu.

Je lakini nini zaidi kinafanyika? Ungana na Assumpta Massoi katika makala hii.