Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Dola milioni 29 zahitajika kunusuru watu wa Vanuatu.

Dola milioni 29 zahitajika kunusuru watu wa Vanuatu.

Changisho la dharura limezinduliwa leo kwa ajili ya kusaidia zaidi ya nusu ya idadi ya watu nchini Vanuatu walioathiriwa na kimbunga PAM kilichoikumba nchi hiyo siku 11 zilizopita.

Changisho hilo linataka jumuiya ya kimataifa kuchangia zaidi ya dola miloni 29 ili kusaidia serikali katika kukabilina na athari za kimbunga PAM ambapo zaidi ya watu elfu 70 wanahitaji msaada wa dharura wa malazi huku zaidi ya watu laki moja wakihitaji maji safi ya kunywa kutokana na kuharibika kwa vyanzo vya maji.

Akiongea na waandishi wa habari mjini Geneva msemaji wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Usaidizi wa Kibinadamu, OCHA Jans Laerke anasema..

(SAUTI JAN)

"Kipaumbele cha juu cha msaada huu ni kutoa huduma muhimu zenye  kuokoa maisha  kama vile chakula, maji, huduma za afya na makazi katika maeneo yote yaliyoathirika, lakini pia ni kusaidia watu kurejesha maisha yao ya zamani na kuanzisha upya huduma za msingi, kama vile elimu."