Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kifua Kikuu bado ni tishio tuchukue hatua:WHO

Kifua Kikuu bado ni tishio tuchukue hatua:WHO

Leo ni siku ya Kifua Kikuu, TB, duniani ambapo Shirika la Afya Duniani, WHO linataka utekelezaji wa mkakati utakaotokomeza vifo vitokanavyo na Kifua Kikuu, wagonjwa sambamba na machungu yatokanayo na ugonjwa huo ili kuendeleza mafanikio yaliyopatikana kupitia utambuzi mapema wa wagonjwa. Taarifa zaidi na Amina Hassan.

(Taarifa ya Amina)

Mkakati huo unataja misingi mikuu mitatu ya kuzingatiwa na wadau wakuu kwenye mpango huo ambao ni serikali, wadau wa kimataifa, mashirika yasiyo ya kiserikali na jamii.

Misingi hiyo ni mosi, wagonjwa kuwa kitovu cha huduma, pili sera thabiti, na tatu tafiti na mbinu bunifu ili kukabiliana na ugonjwa huo.

Je nchini Tanzania hali ikoje, Dkt. Beatrica Mutayoba ni mkuu wa mpango wa Kifua Kikuu na Ukoma nchini humo.

(Sauti ya Dkt. Mutayoba)

Halikadhalika amezungumzia kinachofanyika kuboresha huduma kwa wagonjwa.

(Sauti ya Dkt, Mutayoba)