Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Amani ni lazima ipatikane Gaza baada ya uharibifu mkubwa- ripoti

Amani ni lazima ipatikane Gaza baada ya uharibifu mkubwa- ripoti

Waisraeli, Wapalestina pamoja na jamii ya kimataifa wana wajibu wa kumaliza uhasama ambao unatishia kulipua mzozo wa mara kwa mara, na kuepusha ukiukaji zaidi wa haki za binadamu, kwa mujibu wa ripoti mypa za Umoja wa Mataifa. Taarifa kamili na Joshua Mmali.

Taarifa ya Joshua

Ripoti kuhusu hali ya haki za binadamu katika maeneo ya Wapalestina yaliyokaliwa zimewasilishwa na Makarim Wabisono, Mtaalam maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya haki za binadamu katika maeneo hayo, na Flavia Pansieri, Naibu Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu katika Umoja wa Mataifa.

Bwana Wabisono amesema kuwa mamia ya watoto walikuwa wahanga wa mapigano hayo, akiongeza kuwa idadi kubwa ya raia waliouawa katika mapigano hayo ilisababisha kuhoji iwapo Israel inaheshimu sheria ya kimataifa ya kibinadamu.

Litakuwa jambo la aibu kupuuza uhai wa wanawake, wanaume na watoto wasio na hatia kama sehemu ya ajali ya vita. Wote walikuwa wahanga wa mzozo unaoendelea , na ni jukumu la Waisraeli, Wapelestina na jamii ya kimataifa kupiga hatua za kuelekea amani na kumaliza machafuko.”

Akiwasilisha ripoti saba za Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu kuhusu hali ya haki za binadamu katika maeneo ya Wapalestina yaliyokaliwa, Naibu wake, Flavia Pansieri amesema hali Gaza inatia hofu, akiitosa Israel kidole cha lawama

Sauti ya Pansieri 1

Matukio kati ya Juni 12 na Agosti 26 mwaka 2014 na madhara yake makubwa, pia yanaibua maswali kuhusu ikiwa Israel inaheshimu wajibu wake chini ya sheria ya kimataifa ya kibinadamu, wa kutofautisha kati ya raia na wapiganaji.”

Amevilaani pia vitendo vya makundi ya Kipalestina yaliyojihami

Sauti ya Pansieri 2

Urushaji maroketi kiholela kwa makazi ya raia wa Israel, pia ni ukiukaji dhahiri wa sheria ya kimataifa ya haki za binadamu na sheria ya kibinadamu.”