Skip to main content

Historia itufunze kukabiliana na ubaguzi wa rangi sasa- Ban

Historia itufunze kukabiliana na ubaguzi wa rangi sasa- Ban

Ikiwa leo ni Siku ya Kimataifa ya Kutokomeza Ubaguzi wa Rangi, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, amesema kuwa kila siku, watu wa kila umri hukumbana na chuki, kunyimwa haki na kudhalilishwa kwa misingi ya rangi ya ngozi, asili yao, utaifa au kabila na aina nyingine za ubaguzi.

Ban amesema kuwa ubaguzi kama huo umekuwa chanzo cha unyanyasaji, umaskini, utumwa, mauaji ya kimbari na vita.

Amesema Siku ya Kimataifa ya Kutokomeza Ubaguzi wa Rangi ni fursa ya kuahidi upya kujenga ulimwengu wenye haki na usawa, na ambako hakuna ubaguzi wa rangi na kuwadharau wengine. Amesema ni lazima kujifunza kutokana na historia na kukubali madhara makubwa yaliyosababishwa na ubaguzi wa rangi.