Skip to main content

Watu milioni 700 hawapati huduma ya maji safi duniani

Watu milioni 700 hawapati huduma ya maji safi duniani

Mwishoni mwa juma Tarehe 22 Machi,ni maadhimisho ya siku ya maji duniani. Siku hii ni fursa ya kumulika umuhimu wa maji kwa ustawi wa jamii. Maadhimisho ya mwaka huu pia yanaangazia matumizi ya vyoo na huduma za kujisafi. Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF linasema licha ya kwamba upatikanaji wa mjai ya kunywa imekuwa ni moja ya mafanikio makubwa katika malengo ya maendeleo ya Milenia MDGS, kuelekea siku hii ya maji bado takwimu zinaonyesha kuwa zaidi ya watu milioni 700 kote duniani hawapati huduma ya maji safi. Hii ni changamoto kubwa!