Ban aongea na Netanyahu baada ya Uchaguzi Israel

Ban aongea na Netanyahu baada ya Uchaguzi Israel

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ameongea kwa njia ya simu na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu akimpongeza kwa kushinda uchaguzi wa hivi karibuni.

Taarifa ya msemaji wa Umoja wa Mataifa imesema Bwana Ban amemwambia Waziri mkuu huyo kwamba anatarajia kushirikiana na serikali mpya itakapoundwa.

Aidha amemsihi Waziri mkuu kuirudishia serikali ya Palestina kipato cha ushuru ambacho kimezuiliwa na Israel kwa kipindi cha miezi kadhaa sasa.

Hatimaye Katibu Mkuu amekariri msimamo wake kuhusu suluhu ya mataifa mawili kama njia ya pekee ya kupata amani na amemsihi Waziri mkuu kurejea uungaji mkono wa Israel kuhusu suluhu hiyo.