Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kutoka CSW59 tunaondoka na mengi: Tanzania

Kutoka CSW59 tunaondoka na mengi: Tanzania

Mkutano wa 59 wa kamisheni ya hali ya wanawake duniani umekunja jamvi kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa baada ya wiki mbili za majadiliano, vikao na tathmini ya maazimio ya Beijingi miaka 20 iliyopita.

Halikadhalika washiriki kutoka nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa waliangalia jinsi ya kuimarisha utekelezaji wa maazimio hayo ya mkutano wa nne wa kimataifa wa wanawake kwenye ajenda ya maendeleo endelevu baada ya mwaka 2015.

Miongoni mwa nchi zilizoshiriki ni Tanzania ambapo Assumpta Massoi wa Idhaa hii alipata fursa ya kuzungumza na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Anna Maembe punde tu baada ya kutoa mada kwenye mkutano uliongalia jinsi ya kuhakikisha hakuna anayechwa nyuma kuelekea maendeleo endelevu baada ya mwaka 2015.

Hapa anaanza kwa kusema kile walichojadili…