Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Morocco yapokea viongozi wa Libya kwa ajili ya mazungumzo ya amani

Morocco yapokea viongozi wa Libya kwa ajili ya mazungumzo ya amani

Awamu nyingine ya mazungumzo ya kisiasa kati ya wadau wote wa Libya imeanza leo nchini Morocco.Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Libya UNSMIL, ambao unaratibu mazungumzo hayo, umesema katika taarifa yake kwamba washiriki wa mazungumzo watajadili kuhusu uundwaji wa serikali jumuishi, utaratibu wa kurejesha usalama hasa mji mkuu Tripoli na kujisalimisha kwa vikundi vilivyojihami.

UNSMIL imeongeza kuwa wadau wote wamefika kwenye mazungumzo na moyo wa uwazi, maridhiano na utashi wa kufikia makubaliano yatakayorudisha amani ya kudumu nchini Libya.

Mazungumzo haya yameanza wakati ambapo mashambulizi ya kigaidi yamelenga viwanja vya ndege nchini Libya, siku ya jumatano na alhamisi, UNSMIL ikisema kwamba lengo la watekelezaji wa uhalifu huo lilikuwa ni kuchelewesha washiriki wa mazungumzo hayo na kuyumbisha utaratibu wa amani.