Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban alaani mashambulio ya Ijumaa huko Yemen

Ban alaani mashambulio ya Ijumaa huko Yemen

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amelaani vikali mashambulio ya kigaidi yaliyofanyika siku ya Ijumaa na kusababisha vifo vya watu kadhaaa huku wengine wangi wakijeruhiwa.

Mashambulio hiyo yamefanyika wakati wa swala ya Ijumaa kwenye misikiti miwili iliyoko mji mkuu, Sana’a, halikadhalika kwenye jengo la serikali na msikiti mwingine huko Sa’dah.

Naibu msemaji wa Umoja wa Mataifa Farhan Haq amemnukuu Ban akituma rambirambi kwa wafiwa na serikali ya Yemen na kutakia ahueni ya haraka majeruhi huku akisema..

“Katibu Mkuu anatoa wito kwa pande zote nchini Yemen kusitisha mara moja chuki baina yao na kujizuia kwa kiasi kikubwa. Pande zote ni lazima zizingatie azma zao za kumaliza tofauti kwa njia ya amani na zishiriki kwa dhati kwenye mashauriano  yanayorajibiwa na Umoja wa Mataifa ili kufikia makubaliano kwa mujibu wa taratibu kadhaa ikiwezo zile za baraza la ushirikiano la nchi za ghuba.”

Katibu Mkuu amekumbusha pande zote nchini Yemen juu ya uwajibikaji wao kwa mujibu wa maazimio ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Mashambulio hayo pia yamelaaniwa vikali na Mshauri maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa huko Yemen Jamal Benomar.