Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uwepo wa wanawake bungeni ni muhimu katika kuendeleza maswala yao:KEWOPA

Uwepo wa wanawake bungeni ni muhimu katika kuendeleza maswala yao:KEWOPA

Tumeweza kupitisha sheria mbali mbali nchini Kenya  zinazoangazia maswala ya wanawake nchini Kenya.

Hiyo ni kauli ya Cecily Mbarire, mwenyekiti wa Muungano wa wanawake wa bunge nchini Kenya, KEWOPA ambayo ametoa kwenye mkutano ulioandaliwa na chama hicho kando mwa mkutano wa 59 wa kamisheni ya  hali ya wanawake duniani, CSW59 unaofikia ukomo leo.

Amesema sheria ya upendeleo maalum ya kuhakikisha wanaume  sio zaidi ya theluthi mbili katika bunge imewezesha kupaza sauti maswala ya wanawake

(Sauti ya Mbarire)

Kwa upande wake mbunge mteule Seneta Elizabeth Ongora- Masha amesema kuteuliwa kwa wanawake ni ishara ya kuwepo kwa pengo

(Sauti ya Elizabeth)