Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Utumikishaji watoto jeshini Sudan Kusini waendelea:UNICEF

Utumikishaji watoto jeshini Sudan Kusini waendelea:UNICEF

Mustakhbali wa watoto nchini Sudan Kusini umesalia mashakani hasa kwenye majimbo ya Upper Nile na Unity kutokana na watoto kuendelea kutumikishwa vitani. Hiyo ni kwa mujibu wa shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa, UNICEF. Taarifa zaidi na Amina Hassan.

(Taarifa ya Amina)

UNICEF inasema watendaji wake pamoja na wadau walioko eneo hilo wameripoti ongezeko la uandikishaji watoto jeshini mwezi uliopita kunakofanywa na serikali na kikundi cha Johnson  Olomi.

Mwakilishi wa UNICEF huko Sudan  Kusini Jonathan Veitch amewaambia waandishi wa habari Geneva, Uswisi kuwa utumikishaji watoto hawajaachiliwa huru licha ya maombi ya kutaka pande hizo zifanye hivyo.

Amesema watoto wanaoshikiliwa wanaruhusiwa kwenda nyumbani mchana lakini jioni ni lazima warejee kambini na la kusikitisha zaidi..

Uthibitishaji wa idadi na kile kinachokumba watoto imekuwa vigumu kutokana na vitisho dhidi ya watu na mashirika yanayojaribu kufuatilia hali ilivyo. Ikichukuliwa pamoja tunaamini idadi ya watoto waliotekwa huko Unity na Upper Nile mwezi uliopita inafikia mamia kwa mwezi uliopita.”

UNICEF imekumbusha serikali na upinzani Sudan Kusini kuwa utumikishaji watoto jeshini ni ukiukwaji mkubwa wa haki zao za msingi na kwamba warejelee makubaliano waliyosaini ya kuacha kutumikisha watoto.