Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ilibidi kufanya maamuzi magumu kutokomeza Ebola : Rais Sirleaf

Ilibidi kufanya maamuzi magumu kutokomeza Ebola : Rais Sirleaf

Rais wa Liberia Ellen Johson Sirleaf amesema nchi yake ililazimika kufanya maamuzi magumu kwa kusema yatosha hatua iliyofanikisha kutokomeza homa kali ya Ebola iliyoikumba nchi hiyo ya Afrika Magharibi mwaka jana.

Katika mahojiano maalum na Joseph Msami wa idhaa hii mjini New York, Rais Sirleaf amesema hali likuwa ya kutisha hasa kwa kuzingatia kuwa watu walikuwa hawana elimu yoyote kuhusu Ebola na hivyo kukimbia hovyo.

(SAUTI ELLEN)

"Watu hawakujua nini cha kufanya , hawakujua adui huyu alikuwa ni nini na hata namna ya kukabiliana naye. Ilikuwa inatisha sana. Lakini ilitupa ujasiri, unapokabiliana na hili unajipima na kuamka. Watu wa Liberia, asasi za kiraia mashirika ya vijana na wanawake na hata ya kidini waliamka nakusema hatutakubali kushindwa na adui huyu asiyejulikana."

Usikose mahojinao zaidi na kiongozi huyu wa kwanza mwanamke kuwa Rais wa kuchaguliwa barani Afrika mwishoni mwa juma katika ukurasa wetu