Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tuko tayari kwa majadiliano na Umoja wa Mataifa: DRC

Tuko tayari kwa majadiliano na Umoja wa Mataifa: DRC

Serikali ya Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, DRC, imesema imejizatiti kuhakikisha uchaguzi ujao unakuwa wa kidemokrasia.

Hakikisho hilo limetolewa na Waziri wa Mambo ya Nje wa DRC Raymond Tshibanda alipohutubia baraza la usalama siku ya alhamisi wakati wa kikao kuhusu hali inayoendelea nchini humo.

(Sauti ya Tshibanda)

“Na ndio maana baada ya mjadala wa wazi na wa kutosheleza Tume huru ya Taifa ya uchaguzi imechapisha kalenda ya uchaguzi. Ni nia yetu kuandaa chaguzi za wazi, halali na huru. Tunatumaini kuwa marafiki wa DRC watashirikiana nasi katika zoezi hili tunapojifunza zaidi na kujielimisha kuhusu demokrasia na mazingira ya amnai na kuepuka muingiliano wowote unaoweza kuchochea moto.”

Katika hotuba yake Waziri huyo wa Mambo ya Nje wa DRC alitaja mambo manne ambayo amesema yameibua mvutano uliopo sasa katika serikali hiyo na Umoja wa Mataifa.

Mambo hayo ni mkakati wa kuhamisha majukumu ya MONUSCO na kasi ya kupunguza vikosi vya Umoja wa Mataifa nchini humo, pilli upokonyaji silaha waasi wa FDLR, tatu uwepo wa vikundi vya ADF kaskazini mashariki mwa DRC na Nne athari za kisiasa baada ya kutokomezwa kwa kikundi cha M23.

Hivyo mwishoni amesema…

(Sauti ya Tshibanda)

“Ningependa kusema kuwa tuko tayari kuingiakwenye majadiliano ya kimkakati na Umoja wa Mataifa katika mambo yote manne niliyotaja kwa lengo la kufikia makubaliano kabla Baraza halijatoa uamuzi.”