Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WFP yazindua mpango mpya wa vocha za vyakula CAR

WFP yazindua mpango mpya wa vocha za vyakula CAR

Shirika la Mpango wa Chakula Duniani(WFP) limeanza mpango wake wa kwanza wa vocha za chakula nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR ili kusaidia watu zaidi ya 100,000 wanoatahiriwa na machafuko.

Mpango huu wa hutoa mwanya kwa wapokeaji kuchagua vyakula vya asili. Mustapha Darboe ni mwakilishi wa WFP nchini CAR.

(Sauti ya Darboe)

Kwa mujibu wa WFP mpango huu hutoa mwanya kwa wapokeaji kuchagua vyakula vya asili kama vile kunde, mchele na mafuta.

Mpango huu wa vocha hizo zenye thamani ya dola 10 utafikia maeneo ya mji mkuu Bangui na kwingine,  katika kipindi cha miezi sita ambapo masoko yamefunguliwa nakufanya kazi kama kawaida licha ya ukosefu wa usalama.

Mmoja wa watu 500 waliopoteza makazi katika eneo litwalo Yaloke amenukuliwa akisema sehemu kubwa ya mifugo imeibiwa wakati wa machafuko na hivyo mpango wa vocha za vyakula kutoka WFP utawasaidia kupata maziwa kwa ajili ya watoto wao na kupata chakula wakitakacho.