Tathmini ya uharibifu wa kimbunga Pam yaonyesha mahitaji zaidi
Tathmini ya pamoja inayoongozwa na serikali ya Vanuatu ikishirikiana na mashirika ya kibinadamu, imefikia maeneo mapya, hususan yale yaliyoathiriwa zaidi na kimbunga Pam, yakiwemo Malampa, Penama, Shefa na Tafea. Inakadiriwa kuwa nyumba zipatazo 30,000 ziliharibiwa na kimbunga hicho katika maeneo yaliyoathiriwa zaidi.
Tathmini hiyo imeonyesha kuwa chakula, maji, vifaa tiba, makazi na vifaa vya kujisafi ndivyo vitu vinavyohitajika zaidi, kwa mujibu wa Ofisi ya Kuratibu Misaada ya Kibinadamu, OCHA.
Kwa mujibu wa Ofisi ya kitaifa ya kudhibiti majanga Vanuatu, idadi ya watu waliothibitishwa kufariki dunia kufikia sasa ni 11, huku watu wapatao 3,026 wakiwa wametafuta makazi katika vituo 36 vya uokozi mji mkuu Port Vila. Hata hivyo, OCHA imesema idadi ya watu katika vituo hivyo imeanza kupungua, kwani wengine wameanza kurejea nyumbani.ungu awasadie sana.