Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vikundi vya ugaidi na uhamiaji haramu vyamtia hofu Ban

Vikundi vya ugaidi na uhamiaji haramu vyamtia hofu Ban

Akiwa ziarani nchini Italia Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban ki- Moon ameelezea kusikitishwa kwake na kuongezeka kwa kundi la kigaidi  linalotaka uwepo wa  dola la kiisilamu ISIL au Daesh nchini Libya.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Roma, Ban ameitaka nchi hiyo kusaidia katika juhudi za kutafuta suluhu Libya.

Kadhalika Katibu Mkuu akamulika suala la wahamiaji haramu wengi wao wakiwa ni kutoka barani Afrika ambapo amepongeza Italia kwa juhudi za kuwanusuru na akisema,

(SAUTI)

“Nimetishwa na vitendo dhalimu vinavyofanywa na wasafirishaji haramu kwa wahamiaji, wasaka hifadhi na wakimbizi kwa kuwanyanyasa na mara nyingi kuwatosa baharini na kuwaua. Nautaka Umoja wa Ulaya na nchi nyingine kujihusisha zaidi katika kutatua changamoto hii.