Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la Usalama lajadili hali Darfur na UNAMID

Baraza la Usalama lajadili hali Darfur na UNAMID

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, leo limekutana kuhusu hali katika jimbo la Darfur, Magharibi mwa Sudan, ambapo limesikiliza ripoti mbili za Katibu Mkuu kuhusu Ujumbe wa pamoja wa Umoja wa Mataifa na Muungano wa Afrika Darfur, UNAMID. Amina Hassan na maelezo zaidi..

(Taarifa ya Amina)

Ripoti hizo mbili zimewasilishwa na Herves Ladsous, Mkuu wa Operesheni za Ulinzi wa Amani katika Umoja wa Mataifa. Ripoti ya Februari 26 imesema kuendelea kwa vitendo vya makundi yenye silaha vimesababisha kuzorota kwa hali ya kibinadamu hata zaidi, zaidi ya watu 450,000 wakiwa wamelazimika kuhama makwao katika mwaka 2014 pekee.

(Sauti ya Ladsous)

“Hii ndiyo idadi kubwa zaidi katika mwaka mmoja tangu kilele cha mapigano 2004. Kati yao, 300,000 bado wanaishi katika kambi za wakimbizi wa ndani. Idadi ya wakimbizi Darfur sasa ni zaidi ya milioni 2.5.”

Ripoti ya Machi 13 inataja mafanikio ya ujumbe wa UNAMID, yakiwemo kuanza mchakato wa amani na ulinzi wa raia, huku ikitaja pia changamoto changamoto zilizopo.

Ripoti hiyo pia inaweka bayana mkakati wa kuondolewa kwa ujumbe wa UNAMID, na kuamishia mamlaka yake kwa timu ya kitaifa ya Umoja wa Mataifa.

(Sauti ya Ladsous)

“Inatazamiwa kuwa uhamisho huu utafanyika kwa vipindi tofauti, kwa kuzingatia hali ya usalama Darfur na pia ufadhili na uwezo wa timu hiyo ya kitaifa.”