Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WFP inapeleka msaada wa kiufundi na chakula Vanuatu:

WFP inapeleka msaada wa kiufundi na chakula Vanuatu:

Shirika la mpango wa chakula duniani WFP limeombwa kutoa msaada wa kiufundi, kusimamia misaada na mipango ya ugawaji wa chakula kwa watu walioathirika na kimbunga PAM kisiwani Vanuatu. Grace Kaneiya na taarifa kamili

(TAARIFA YA GRACE KANEIYA)

WFP imesema ina akiba kubwa ya biskuti zenye kutia nguvu na ziko tayari kusafirishwa kwa ndege hadi Vanuatu kama italazimika.

Tathmini ya awali ya WFP inaonyesha kuwa watu 171,000 ambao ni theluthi mbili ya watu wote wa kisiwa hicho wameathirika na kimbunga PAM.

Idadi hii inajumuisha watu 38,000 ambao walikuwa wanaishi kwenye kitovu cha kimbunga hicho, ambao WFP inadhani wameathirika zaidi.

Shirika hilo limesema tathmini yao imefanywa na wataalam wa WFP kutoka mbali kwa hiyo itahitaji kuthibitishwa na ufuatiliaji wa hali ilivyo sasa kisiwani humo. Elizabeth Byrs ni msemaji wa WFP.

(CLIP YA ELIZABETH BYRS)

"Takriban Asilimia 80 ya watu wa Vanuatu wanategemea kilimo. Mazao mengi yameharibika, hasa minazi ambayo imeangushwa . Bado hatujui kiasi cha uharibifu, lakini ni tathmini ya awali. Pia sekta ya uvuvi imeathirika, na ni shida kubwa kwa sababu ni chanzo kipato cha kiuchumi kwa Vanuatu."