Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mifumo bora ya afya yahitajika kupunguza hatari za majanga

Mifumo bora ya afya yahitajika kupunguza hatari za majanga

Mlipuko wa Ebola, mzozo wa Syria au majanga yanayotokea katika maeneo ya Asia-Pasifiki ni mifano inayoonyesha kwamba mifumo bora ya afya ni msingi wa mpango mpya wa kupugunza hatari za majanga unaojadiliwa mjini Sendai, Japan, wamesema leo wataalam wa afya.

Bruce aylward , ambaye ni Mkurugenzi msaidizi wa shirika la Afya duniani, WHO, amesema ili kuvumilia majanga, ni lazima raia wawe na afya nzuri, ambayo itawasaidia kupona haraka.

Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kongamano la tatu la kupunguza hatari za majanga mjini Sendai, Japan, Daktari Aylward amesema pia ni muhimu kutambua hatari za afya zitokanazo na majanga kama mfano kipindupindu.

Bwana Aylward amesema wajumbe wa kongamano hilo wameliweka kipaumbele swala la afya, wakijadili jinsi ya kuimarisha vituo vya afya. Siyo tu kupitia majengo, amesema akiongeza kwamba umuhimu ni kuweza kutoa huduma za afya wakati ambapo majanga yanatokea.