Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hepatitis B yapatiwa mwongozo mpya:WHO

Hepatitis B yapatiwa mwongozo mpya:WHO

Shirika la Afya Duniani, WHO, leo kwa mara ya kwanza limetoa mwongozo wake wenye mapendekezo sita kuhusu matibabu ya homa ya ini aina ya Hepatitis B. Taarifa zaidi na Assumpta Massoi.

(Taarifa ya Assumpta)

Homa ya Hepatitis B hutokana na kirusi kinachoambukizwa kupitia kwenye damu na majimaji mengine ya mwili, na ambacho huvamia ini na kusababisha vifo vya watu wapatao 650,000 kila mwaka, wengi wao wakiwa katika nchi za kipato cha chini na kipato cha wastani.

Inakadiriwa kuwa watu milioni 240 kote duniani wana kirusi cha Hepatitis B, idadi kubwa ya maambukizi ikipatikana bara Afrika na Asia.

Mwanasayansi kutoka WHO Dkt. Phillipa Easterbrook anataja baadhi ya mapendekezo ya mwongozo huo.

(Sauti ya Dkt.Easterbrook)

"Jinsi ya kutafiti homa imeenea kwa kiasi gani, Kuamua nani anahitaji matibabu, Matibabu yapi yatumike awali na yapi yafuatie ikiwa ya awali hayakufanya kazi, na pia jinsi ya kufuatilia mambo manne ambayo ni kuangalia kama kuna saratani ya ini, na  kiasi gani ugonjwa wa ini unavyoendelea. Kuangalia kama matibabu yanafanya kazi na madhara yaletwayo na tiba hiyo."