Tukimwezesha mwanamke wa kijijini tutaiwezesha jamii: Bi. Ruto

11 Machi 2015

Wakati mkutano wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake ukiendelea mjini New York, mke wa makamu wa rais wa Kenya Bi.Rachel Ruto, ambaye ni miongoni mwa washiriki, amesema kwamba alianzisha shirika lisilo la kiserikali la Joyful women kwa ajili ya kumwezesha mwanamke wa kijijini.Katika mahojiano na Grace Kaneiya wa Idhaa hii, Bi. Ruto ambaye ni mlezi wa shirika hilo,  amesema kwamba anatambua umuhimu wa mwanamke wa kijijini kwani mamake mzazi kama mwanamke wa kijijini aliwalea watoto wake hadi uzima wao licha ya kwamba alikuwa mjinga wa kutojua kusoma na kuandika. Hapa anaanza kwa kuelezea lengo la shirika lake

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter