Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Zeid ataka hatua za kisheria zichukuliwe dhidi ya washukiwa wa uhalifu Côte d’Ivoire

Zeid ataka hatua za kisheria zichukuliwe dhidi ya washukiwa wa uhalifu Côte d’Ivoire

Kamishna wa haki za binadamu katika Umoja wa Mataifa Zeid Ra’ad Al Hussein ameitaka serikali ya Cote d’Ivoire kuhakikisha wahusika wa vitendo vya ukatili dhidi ya binadamu wakati wa mgogoro baada ya uchaguzi mwaka 2011 wanafikishwa katika vyombo vya sheria na haki kutendeka.Kauli ya Kamishna Zeid inakuja siku chache baada ya wafuasi wa aliyekuwa rais wa nchi hiyo Laurent Gbagbo kushtakiwa kwa makosa dhidi ya serikali na taasisi zake. Ametaka haki itendeke kwa washukiwa hao wanaodaiwa kutekeleza uhalifu kabla na wakati wa mgogoro.

Kamishna Zeid amenukuliwa akisema kuwa wahanga wa matukio makubwa ya uhalifu wa haki, mengine yakitajwa kuwa yanaweza kuchochea vita na uhalifu dhidi ya ubinadamu, bado hawajaona haki ikitendeka miaka minne baada ya mgogoro nchini Côte d’Ivoire.

Ameelezea kushangazwa kwake kwamba hakuna hata mmoja kati ya washukiwa ambaye amefikishwa mahakamani huku wengine bado wakishikilia nafasi za majukumu nchini humo na kuitaka hatua za haraka zichukuliwe bila kuchelewa.