Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la usalama lalaani shambulio la kigaidi, Mali

Baraza la usalama lalaani shambulio la kigaidi, Mali

Wanachama wa baraza la Usalama wamelaani vikali shambulio la kidaidi lililotokea leo kwenye mji mkuu Bamako, nchini Mali, ambapo watu 5 wamefariki dunia na wengine saba wamejeruhiwa.

Miongoni mwa majeraha ni wafanyakazi wawili wa Umoja wa Mataifa.

Wanachama wa Baraza la Usalama wamepeleka salamu zao za rambirambi kwa familia za wahanga na serikali za Mali, Ufaransa na Ubelgiji, pamoja na kuwatakia nafuu waliojeruhiwa.

Halikadhalika, wakilaani aina zote za vitendo vya ugaidi, wamesisitiza umuhimu wa kupambana navyo kwa kuheshimu haki za binadamu.

Naye Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amepeleka rambirambi zake kwa familia za wahanga akitaka uchunguzi ufanywe haraka iwezekanavyo na watekelezaji wa uhalifu huo wapelekwe mbele ya sheria.

Aidha amekaribisha hatua zilizochukuliwa mapema na serikali ya Mali pamoja na Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo.