Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Muziki watumainisha mustakhabali bora baada ya Ebola

Muziki watumainisha mustakhabali bora baada ya Ebola

Katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa, mjini New York, wadau walioshirikiana katika juhudi za kimataifa dhidi ya mlipuko wa Ebola huko Afrika Magharibi wamekutana hivi karibuni katika tumbuizo maalum. Tumbuizo hilo lilileta pamoja wasanii kutoka maeneo mbalimbali hususan Afrika Magharibi, ambao pamoja na kuburudisha na kuelezea hali halisi ya Ebola, walipata fursa ya kusikiliza uzoefu wa viongozi wa mashirika ya kimataifa na jamii kwenye harakati dhidi ya Ebola na pia kuzindua wimbo maalum wa kuleta matumaini.

Kulikoni? Priscilla Lecomte alihudhuria burudani hiyo, ungana naye kwenye makala hii.