Skip to main content

Mashirika ya UM yakutana kujadili usalama wa wahamiaji baharini:IMO

Mashirika ya UM yakutana kujadili usalama wa wahamiaji baharini:IMO

Mashirika ya Umoja wa Mataifa yamekutana leo Jumatano mjini London Uingereza kujadili njia za kushughulikia idadi kubwa ya maisha ya watu yanayopotea kila uchao baharini kutokana na safari zisizosalama , hususan kwenye bahari ya Mediteranian ambako mamia ya watu wamearifiwa kufa maji katika wiki za karibuni pekee wakiwa katika safari za hatari kutaka kuingia Ulaya. Taarifa kamili na Flora Nducha.

(Taarifa ya Flora)

Mwenyeji wa mkutano huo wa ngazi ya juu ni makao makuu ya mjini London ya shirika la kimataifa la kimataifa la masuala ya majini (IMO) na lengo ni kusaidia majadiliano na kuchagiza ushirikiano na mshikamano baiana ya mashirika ya Umoja wa Mataifa, mashirika ya kimataifa, mashirika yasiyo ya kiserikali (NGO’s), serikali na sekta ya usafiri wa majini.

Katika mkutano huo wamekubaliana kuanzisha utaratibu itakaokuwa imara, na kuongeza ushirikiano wa mawasiliano baina ya mashirika na wadau wengine huku wakiheshimu masuala wahamiaji mchanganyiko.

Mkutano pia unajadili miradi ya pamoja kwa mfano kuanzisha hifadhidata ya pamoja ili kushirikiana taarifa na takwimu kuhusu uhamiaji usiokuwa wa kawaida na vyombo vinavyowasafirisha wahamiaji kwa usafiri usio salama.

Katibu Mkuu wa IMO, Koji Sekimizu amesema hali ya wahamiaji wanovuka bahari katika miaka ya karibuni limefurutu ada na kuwa suala gumu saana katika kujaribu kuwasaidia wahamiaji hao.