Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Taasisi ya Jane Goodall na uwezeshaji watoto wa kike Tanzania

Taasisi ya Jane Goodall na uwezeshaji watoto wa kike Tanzania

Harakati za kumkomboa mwanamke zinaendelea kila uchao maeneo mbali mbali duniani. Umoja wa Mataifa kwa kushirikiana na nchi wanachama pamoja na mashirika yasiyo ya kiserikali wanahaha kuhakikisha wanakomboa kundi hili ambalo idadi yake nusu ya wakazi wote duniani.

Mathalani nchini Tanzania, taasisi ya Jane Goodall kupitia mradi wakewa Fahari ya kuwa msichana unaotekelezwa na programu ya Roots and Shoots imekuwa mstari wa mbele kuwezesha watoto wa kike ili pindi wanapokuwa watu wazima waweze kutimiza wajibu wao kwa manufaa yao na jamii nzima kwa ujumla.

Je nini wanafanya? Stella Vuzo wa kituo cha  habari za Umoja wa Mataifa nchini Tanzania amezungumzo na Catherine Fidelis kutoka mradi  huu na anaanza kwa kufafanua kile wanachofanya.