Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Siku ya kwanza ya kimataifa ya utumaji pesa kuadhimishwa Machi 15: IOM

Siku ya kwanza ya kimataifa ya utumaji pesa kuadhimishwa Machi 15: IOM

Mkuu wa shirika la kimataifa la uhamiaji nchini Uingereza Clarissa Azkoul ameungana na waziri wa kazi wa zamani wa nchi hiyo ambaye pia ni mbunge Dame Tessa Jowell , balozi wa Colombia nchini humo Nestor Osorio na wadau wengine wanaondesha shughuli za utumaji pesa kwenye uzinduzi wa “Siku ya kwanza ya utumaji pesa duniani” ambayo itaadhimishwa rasmi hapo Machi 15 mwaka huu.

Siku ya utumaji pesa duniani itawaleta pamoja wanachama wa sekta ya kutuma fedha pamoja na mashirika ya jumuiya za ughaibuni kama sehemu ya juhudi za kupunguza gharama za utumaji pesa na kuelimisha wateja juu ya chaguo walilonalo katika sekta hiyo isiyo na uwazi na ambayo awali haikuwa na ushindani.