Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNSMIL yatangaza awamu ya pili ya majadiliano ya kusaka amani Libya

UNSMIL yatangaza awamu ya pili ya majadiliano ya kusaka amani Libya

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa usaidizi nchini Libya UNSMIL, umetangaza kuwa awamu ya pili ya majadiliano ya kisiasa itafanyika mwishoni mwa juma hili nchini Morroco baada ya pande alikwa kukubali kushiriki.

Taarifa ya UNSMIL inasema pande husika zimethibitisha ushiriki wao baada ya kufanya mashauriano ya kina na mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu Bernardino Leon wakati wa ziara yake huko Tobruk na mji mkuu Tripoli mnamo March 2 mwaka huu.

Kadhalika pande hizo zimekwenda mbali zaidi na kusisitiza umuhimu wa kufufua mchakato wa majadiliano hima kwa kuwa ni njia pekee ya kutafuta suluhu katika mzozo wa kisiasa wa Libya na hivyo kukomesha kabisa madhila yanayowakumba wananchi wa taifa hilo.

Katika hatua nyingine washiriki wa majadiliano hayo ya kutafuta suluhu wamelaani sahmbulio la kigaidi huko Qubbah mnamo Februari 20 lililosababisha upotevu wa maisha ya watu wasio na hatia.