Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Rasi ya Korea imejizatiti kinyuklia aonya mjumbe wa DPRK

Rasi ya Korea imejizatiti kinyuklia aonya mjumbe wa DPRK

Waziri wa mambo ya nje wa Jamhuri ya watu wa Korea DPRK Ri Su Yong ameonya Jumanne kwamba taifa lake lina uwezo wa kufanya shambulio la nyuklia kabla ya muafaka endapo italazimika , kabla atalielezea taifa hilo kuwa kwa upande wa nyuklia ni “kugusa na kwenda”.

Katika mazungumzo ya upokonyaji wa silaha yaliyoandaliwa na Umoja wa Mataifa mjini Geneva wiki hii mwakilishi huyo wa DPRK ameikosoa Marekani kwa miongo ya vitisho , na kusema kwamba Marekani ndiyo ya kulaumiwa endapo uadui utazuka.

Mjumbe huyo amesema Marekani ni taifa kubwa la silaha za nyuklia na Korea ya Kaskazini ni taifa changa la silaha za nyuklia wakikabiliwa na hali ya vita. Pia ameilaumu Marekani kwa nusu karne ya ushirika wa kijeshi na Korea ya Kusini.

Akiongeza kuwa wakati mvutano unaongezeka baina ya nchi yake na Marekani , taifa lake halitoachana na haki yake ya kujilinda na kujitetea.

Kwa upande wake Marekani imesema imekuwa ikiendesha mazoezi ya kijeshi kwa kushirikisha mataifa 10 nchi wanachama kila mwaka kwa miaka 40 iliyopita. Balozi Robert Wood amesema Marekani haitoikubali Korea Kaskazini kama taifa la nyuklia na imelitaka taifa hilo kuheshimu wajibu wake wa kimataifa.