Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Raia walindwe katika operesheni dhidi ya ISIL Iraq: Mladenov

Raia walindwe katika operesheni dhidi ya ISIL Iraq: Mladenov

Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Iraq Nickolay Mladenov amevitaka vikozi vyote mjini Tikrit nchini Iraq kufanya kila wawezalo kuwalinda raia kwa mujibu wa viwango vya kimataifa.

Bwana Mladenov amekaririwa akisema kuwa operesheni za kijeshi zinazotekelezwa na vikosi vya kimataifa na vile vya Iraq lazima zinaendeshwa kwa uangalifu wa hali ya juu na kwa heshima kwa haki za binadamu na sheria za kimataifa za vita.

Pia ametaka serikali na jumuiya ya kimataifa kuchukua hatua za dharura kuhakikisha kuwa wanaohitaji misaada ya kibinadamu wanapatiwa ili wale waliokimbia kundi la dola ya kiislamu ISIL, warudishwe salama majumbani.