Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watanzania wapata habari kuhusu Ebola kupitia simu za mkononi

Watanzania wapata habari kuhusu Ebola kupitia simu za mkononi

Nchini Tanzania, Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto UNICEF limezindua kampeni ya kuhamasisha jamii kuhusu Ebola kupitia ujumbe wa simu za mkononi kwa ushirikiano na wizara ya afya na kampuni ya Push Mobile.

Mwakilishi wa Kudumu wa Umoja wa Mataifa nchini Tanzania Alvaro Rodriguez ameiambia Idhaa hii kuwa hata kama mlipuko wa Ebola unaanza kudhibitiwa Afrika ya Magharibi, bado mtu mmoja akisafiri na ugonjwa huu anaweza kuhatarisha jamii nzima.

(Sauti ya Rodriguez)

Amesema teknolojia hii mpya itaweza kutumiwa ili kuelimisha jamii kuhusu mambo mengine yanayohusu haki zao.

Ameongeza kwamba simu za mkononi ndio njia bora ya kufikia jamii akieleza kwamba sasa hivi nchini Tanzania idadi ya simu imezidi mara tatu idadi ya vyoo.

Mradi huu unalenga kuwafikia watanzania milioni 10 kupitia ujumbe kwa kiingereza au kiswahili. Rogriduez ametaja mfano wa ujumbe unaotumiwa:

(Sauti ya Rodriguez)