Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNFPA yatumia michezo katika kampeni dhidi ya mimba za utotoni

UNFPA yatumia michezo katika kampeni dhidi ya mimba za utotoni

Katika kukukuza kampeni dhidi ya mimba za  utotoni, ukeketaji na unyanyasaji kwa watoto Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu UNFPA nchini Tanzania limeshiriki katika mashindano ya riadha ya Kilimanjaro Marathon nchini humo.

Fatina Kiluvya ni mtaalamu wa afya ya vijana wa UNFPA.

(SAUTI FATINA)

Naye mmoja wa wasichana washiriki katika mbio hizo kutoka jamii ya kimasai anaeleza namna alivyonusurika katika ndoa ya utotoni.

(SAUTI MSICHANA)

UNFPA imetumia michezo ili kupenyeza ujumbe kwa kasi kwa kuzingatia takwimu zinazoonyesha kuwa kati ya watoto watano, wawili huolewa wakiwa chini ya miaka 18