Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

De Mistura atuma ujumbe Aleppo huku akishauriana na Syria

De Mistura atuma ujumbe Aleppo huku akishauriana na Syria

Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa kwenye mzozo wa Syria, Staffan De Mistura anaendelea na mashauriano na serikali ya Syria kuhusu suala la kusitisha mapigano kwenye mji wa is Aleppo.

Taarifa ya Umoja wa Mataifa iliyotolewa kwa waandishi wa habari imesema harakati hizo zinaendelea wakati BwanaDe Mistura amepeleka ujumbe kwenye eneo hilo.

Amesema ujumbe huo utatathmini hali ilivyo kwenye eneo hilo na kuhakikisha kuwa pindi usitishaji mapigano unakubaliwa misaada ya kibinadamu inaweza kuongezwa vya kutosha.

Halikadhalika amesema ujumbe utaandaa taratibu zitakazofuatwa iwapo usitishwaji huo utakiukwa.

Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa mzozo wa Syria tangu uanze mwaka 2011 umesabisha watu Milioni 7.6 wapoteze makazi yao huku watu Milioni 12.2 wakihitaji usaidizi wa kibinadamu.