Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Aina zote za ubaguzi hazikubaliki : Ban

Aina zote za ubaguzi hazikubaliki : Ban

Ubaguzi ni ukiukwaji wa haki za binadamu na haupaswi kuachwa uendelee, amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataiaf Ban ki-moon katika ujumbe wake wa kuadhimisha siku ya kimataifa ya kupinga ubaguzi inayoadhimishwa kila tarehe Mosi mwezi Machi.

Siku hii inalenga kutoa ujumbe kwa jumuiya ya kimataifa ili kutokomeza aina zote za ubaguzi ambapo mamilioni ya watu huathiriw na vitendo hivyo kote duniani. Kauli mbiu ya maadhimihso ya mwaka  huu ni Funguka Jitokeze.

Akitoa ujumbe wake kuhusu siku hii Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Ukimwi UNAIDS Michel Sidibé amesema changmoto kuu zinazoikabili dunia zinaweza kutatuliwa kwa kukomesha unyanyapaa na ubaguzi.

Katika kuadhimisha siku hii nguli mbalimabli akiwamo msakata kabumbu wa Brazil David Luiz ambaye ni balozi mwema wa UNAIDS ametoa ujumbe maalum wa kupinga ubaguzi wa rangi.

Luisa Cabal ni mkuu wa haki za binadamu katika shirika la Umoja wa Mataifa la mapambano dhidi ya Ukimwi UNAIDS.

(SAUTI LUISA)