Ban ashtushwa na mauaji ya Nemstov

28 Februari 2015

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ameeleza kushtushwa kwake na mauaji ya kiongozi wa upinzani nchini Urusi, Boris Nemstov kwenye mji mkuuwa, Moscow, sikuya Ijumaa.

 Taarifa ya msemaji wa Umoja wa Mataifa imesema Katibu Mkuu anatambua kutangazwa kuanza kwa uchunguzi wa tukio hilo.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari, inadaiwa kuwa Nestov ambaye aliwahi kushika wadhifa wa Naibu Waziri Mkuu wa shirikisho la Urusi miaka ya 1990, aliuawa na mtu ambaye hadi sasa hajafahamika wakati anavuka daraja moja mjini Moscow.

Ban pamoja na kutuma salamu za rambirambi kwa familia na wafuasi wa marehemu Nestov, amesema ni matumaini yake kuwa watuhumiwa wa tukio hilo watafikishwa mbele ya sheria haraka iwezekanavyo.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter