Ban aendelea kulaani mashambulizi ya Boko Haram dhidi ya raia

27 Februari 2015

Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-moon amerejelea kulaani vikali muendelezo wa mashambulizi ya kulenga raia yanayofanywa na kundi la Boko Haram nchini Cameroon, Chad, Niger na Nigeria.

Ban ameongeza kuwa vitendo vya kuwateka na kuwatumia watoto ikiwemo katika mashambulizi ya kujitoa muhanga ni ukatili na uadui mkubwa dhidi yao. Ban amesema anatiwa moyo na hatua zilizochukuliwa na nchi zinazozungukwa na ziwa Chad ikiwemo Benin kwa msaada Umoja wa nchi za afrika AU za kuunda jeshi maalumu la kukabiliana tishio la Boko Haram katika eneo hilo.

Ametoa wito kwa wadau wa kimataifa kusaidia katika juhudi hizo za kikanda na kuyataka mataifa husika kuhakikisha hatua zote zinazochukuliwa kukabiliana na tishio la kikaidi la Boko Haramu zinazingatia sheria za kimataifa za haki za binadamu, ubinadamu na sheria za wakimbizi.

 

Shiriki kwenye Dodoso UN News 2021:  Bofya hapa Utatumia dakika 4 tu kukamilisha dodoso hili.

♦ Na iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter