Burundi ikielekea uchaguzi mkuu , Umoja wa Mataifa wataka utulivu
Taifa la Burundi lilioko Afrika Mashariki , linajiandaa kwa uchaguzi mkuu mwezi mei mwaka huu. Hata hivyo joto la kisiasa limeanza kupanda miezi mitatu kabla ya zoezi hilo. Shughuli ya kuwaorodhesha wapiga kura katika daftari la wapiga kura, imemalizika chini ya mvutano mkubwa kati ya serikali na upinzani.Baada ya kufungwa rasmi kwa ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Burundi BNUB mwanzoni mwa mwaka huu, Umoja huo umeunda tume ya uangalizi wa uchaguzi na hivyo kutoa wito wa kufanyika uchaguzi huru na wa haki ili kulinusuru taifa na machafuko kama yale yaliyowahi kutokea nchini humo miaka iliyopita.
Mjumbe maalumu wa katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa kwenye ukanda wa maziwa makuu Said Djinit amesema ufanisi wa uchaguzi huo utakuwa ni njia ya kuimarisha demokrasi na utulivu nchini humo. Je nini kinaendelea na nini kinafanyika ili kufanikisha hilo? kutoka Bujumbura, muandishi wetu wa maziwa makuu Ramadhani Kibuga ametuandalia makala ifuatayo.