Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mataifa ya Afrika Magharibi yadhamiria kukomesha hali ya kutokuwa na utaifa

Mataifa ya Afrika Magharibi yadhamiria kukomesha hali ya kutokuwa na utaifa

Ujumbe unaowakilisha mataifa 15 ya Afrika ya Magharibi kwenye mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu kutokuwa na utaifa wameaihidi kuongeza juhudi ili kukomesha kabisa hali ya kutokuwa na utaifa, hatua ambayo inalengo la kutatua hali inayowakabili maelfu ya watu kwenye ukanda wa Afrika ya Magharibi .Hayo yamesemwa na shirika la Umoja la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR kwenye kilele cha mkutano wa ngazi ya juu ulioandaliwa na Umoja wa mataifa wiki hii nchini Ivory Coast.

Nchi hizo 15 ambazo ni wanachama wa jumuiya ya kiuchumi ya Afrika ya Magharibi ECOWAS wamepitisha azimio lenye lengo la kuzuia, kupunguza na kukomesha kabisa hali ya kutokuwa na utaifa.

Kwa mujibu wa UNHCR azimio hilo linajumuisha vipengee 15 vinavoyataka mataifa hayo ya ECOWAS kukusanya taarifa zinazosababisha kutokuwa na utaifa na idadi ya watu wasio na utaifa katika ukanda wao.

Makadirio yanasema takriban watu 750,000 hawana utaifa hivi sasa au wako katika hatari ya kutokuwa na utaifa kote Afrika ya Magharibi wakiwemo watu 700,000 kwa Ivory Coast pekee.